Friday, March 8, 2013

BREKING NEWS: UHURU KENYATTA ASHINDA URAIS KENYA

** *Ankal akisalimiana na Mhe Uhuru Kenyatta siku za nyuma wakati Rais huyo mteule wa Kenya alipotembelea Tanzania. Leo Tume ya Uchaguzi ya Kenya imemtangaza Mhe Kenyatta kuwa mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais baada ya kupata kura dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mhe Raila Odinga*

Monday, March 4, 2013

Bavicha waiteka mbulu

 

Photo

Hakuna kulala hadi kieleweke!




aikizungumza wakati wa kuchangia hoja za ELIMU, RASILIMALI na UTWALA BORA wakati wa kongamano la VIJANA CHADEMA MBULU.

Saturday, March 2, 2013


Kondomu feki zaanza kuleta madhara Uingereza


 


Kwa ufupi
Zaidi ya kesi 21, 000 za maambukizi mapya zimedaiwa kutambulika kwa mwaka 2011/12.

WAKATI kondomu feki zilizopigwa marufuku  Uingereza mwaka jana zikiwa katika mzunguko nchini Tanzania, kesi za gonjwa la ngono hatari lisilotibika zimeongezeka kwa asilimia 25 Uingereza, huku wataalamu wakionya kwamba ugonjwa huo umekuwa sugu zaidi katika tiba.
Zaidi ya kesi 21, 000 za maambukizi mapya zimedaiwa kutambulika kwa mwaka 2011/12.
Kondomu hizo feki aina ya Trojan na Durex zenye vipele vipele ambazo mwishoni mwa mwaka jana serikali ya Uingereza iliingia katika msako mkali  kusaka mamilioni ya kondomu hizo bandia zilizokuwa zikiuzwa nchini humo miezi 18 iliyopita.
Kirusi kinachoambukiza ugonjwa huo hatari kimetajwa kuwa ni 'Neisseria' ambacho ni tofauti na vingine ambavyo mara nyingi hutibiwa kwa dozi moja tu ya  viuavijasumu (antibiotics) ambayo angalau hufanya kazi kwa asilimia 95 kiufanisi.
Akizungumzia maendeleo ya utafiti wa kondomu hizo nchini , Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Wiwango Tanzania(TBS),Leandri Kinabo  alisema shirika hilo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Ckula na Dawa(TFDA) hivi sasa lipo katika mchakato wa kuhakikisha vipimo halisi vya ubora wa bidhaa hizo vinaangaliwa.
"Hili suala ni nyeti na ni la kiafya na usalama zaidi, hivyo tulikaa kikao na TFDA na tulikubaliana tufanye uchunguzi wa kondom hizi, kwani ni kweli zipo sokoni lakini suala la ubora linatakiwa kuangaliwa," alisema Kinabo.
Aliwataka Watanzania kuwa na subira ili waweze kuchunguza bidhaa hizo kwa umakini zaidi na kwamba baada ya uchunguzi watatoa majibu.
Baada ya gazeti hili  kutaka kujua uhalali wa bidhaa hizo sokoni, Kinabo alisema bidhaa zote zinazoingia bandarini hupimwa, lakini kuna baadhi ya bidhaa ambazo huingizwa kwa njia zisizo halali na mara nyingi huwa feki.
"Inetegemea na lebo ya bidhaa husika, kuna wakati bidhaa inaweza kupimwa na kuonekana kuwa ni salama na kisha kuingizwa sokoni, lakini baada ya muda zikaingia bidhaa feki zenye nembo hiyohiyo, hivyo hilo ni suala la kusubiri vipimo kutoka TFDA," alisema Kinabo.
Tatizo hilo sugu Uingereza limesababishwa kuanzishwa kwa kampeni mpya ya kukabiliana na tishio kubwa la kuongezeka kwa kasi kwa magonjwa hayo nchini Uingereza na Wales ambayo yamedaiwa kusambaa kwa wingi nchini humo na nchi zinazoendelea.
Wataalamu wa Afya wana matumaini mapya baada ya kuanzishwa mpango mkakati wa kuzuia ugonjwa wa gono 'Gonorrhoea Resistance Action Plan' ambayo itaongeza ufahamu wa ugonjwa huo.
Mpango huo ulioanzishwa na shirika la Ulinzi wa Afya, utafuatilia tatizo hilo la kimataifa linaloongezeka kwa kasi tangu kupungua miaka 10 iliyopita.



Bavicha Dar yapania kumbana Kawambwa

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk Shukuru Kawambwa. 
 
Kwa ufupi
“Kwa waraka huu ndugu viongozi, mnaombwa kufanya yafuatayo; kuanza maandalizi ya maandamano haya ya kudai elimu bora kwa vijana wa Tanzania, na pia hatma ya waliofelishwa na Serikali ya CCM kwa kuwasiliana na hao waliofeli katika maeneo yenu ikiwa ni pamoja na kuwaandikisha sahihi zao kama sehemu ya wao kuthibitisha kuitaka Serikali iwajibike

BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha),  limewatumia waraka viongozi wake wote wa mikoa na wilaya, unaowataka kujiandaa na maandamano ya kushinikiza viongozi wa juu katika  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, wakiongozwa na Waziri Dk Shukuru Kawambwa, kujiuzulu.
Pamoja na kushinikiza viongozi hao kujiuzulu, Bavicha pia inaitaka Sserikali  kutangaza matokeo hayo ni janga la Kitaifa na kuiweka elimu kipaumbele cha kwanza katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2013/14.
Hatua hiyo imekuja siku kadhaa baada ya kutangazwa kwa matokeo ya  mtihani wa kidato cha nne, uliofanyika kote nchini  mwaka jana.
Matokeo hayo  yalitangazwa na Waziri wa  Elimu na Mafunzo ya Ufundi,  Dk Kawambwa ambaye alisema zaidi asilimia 60.6 ya wanafunzi waliofanya mtihani huo wamepata sifuri.
Waraka huo ambao Mwananchi ilifanikiwa kuupata jana ukiwa umesainiwa na Katibu Mkuu wa Bavicha,Deogratias Munishi, unawaagiza viongozi hao kufanya maandalizi  ya haraka ili kujiandaa na maandamano kama Dk Kawambwa hatajiuzulu wiki moja ijayo.
“Kwa waraka huu ndugu viongozi, mnaombwa kufanya yafuatayo; kuanza maandalizi ya maandamano haya ya kudai elimu bora kwa vijana wa Tanzania, na pia hatma ya waliofelishwa na Serikali ya CCM kwa kuwasiliana na hao waliofeli katika maeneo yenu ikiwa ni pamoja na kuwaandikisha sahihi zao kama sehemu ya wao kuthibitisha kuitaka Serikali iwajibike” ilisema sehemu ya waraka huo.
Waraka huo pia umewataka viongozi hao kuwahamasisha wananchi kuunga mkono azimio hilo kwa kuwaelimisha vijana na wazazi wao kupitia  vyombo vya habari, mikutano ya hadhara na vikao vya ndani.
Akizungumzia waraka huo, Munishi alisema huo ni mwanzo wa utekelezaji wa azimio alilolitoa hivi karibuni la kuaanda maandamano.

Thursday, February 28, 2013

clouds Fm yaibuka na tuzo ya ubora (superbrands) kwa mara ya tatu mfululizo.


*Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu (kati) pamoja na Mkurugenzi wa Mradi wa Superbrands Afrika Mashariki, Bw Jawad Jaffer kwa pamoja wakimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga kwa Couds Fm redio kuibuka na tuzo hiyo ya ubora kwa mara ya tatu mfululizo. Tukio hilo lilifanyika hivi karibuni katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.* *Mkurugenzi wa Mradi Superbrands Afrika Mashariki, Bw Jawad Jaffer akimkabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa. Joseph Kusaga mara ba... more »

Tuesday, February 26, 2013

Waliofeli kidato cha nne waibuka

Wakutana mjini Iringa kuijadili Serikali
WANAFUNZI waliofeli mtihani wa taifa wa kidato cha nne, wamekutana mjini Iringa. Wanafunzi hao walikutana jana saa tano asubuhi, katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mtakatifu Augustino cha Ruaha (RUCO) kwa uratibu wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu.

Katika mkutano huo, wanafunzi zaidi ya 400 kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa, walijaa ukumbini na wengine walilazimika kusimama nje ya ukumbi kwa kuwa ukumbini hakukuwa na nafasi.

Baada ya mjadala kuanza, baadhi ya washiriki waliokuwa wakipewa nafasi ya kuzungumza, walikuwa wakishindwa kujieleza, badala yake walikuwa wakilia kuonyesha ni kwa jinsi gani wasivyoridhishwa na matokeo yao.

Wengine badala ya kuonyesha masikitiko yao, walikuwa wakiishutumu Serikali wazi wazi kwa kile walichokuwa wakisema kwamba wamefeli kutokana na uzembe uliofanywa na waliosahihisha mitihani yao.

Hata hivyo, wakizungumza katika kikao hicho, wanafunzi hao walisema licha ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuunda tume ya kuchunguza matokeo hayo, ikubali kulegeza masharti ya kujiunga na vyuo vya ufundi na vyuo vinginevyo ili waweze kupata elimu wanayoihitaji.

Mmoja wa wanafunzi hao, Gerald Kiyeyeu, aliyehitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya St. Michael, alisema kwa kuwa baadhi yao wanaamini wamefelishwa, kuna haja kwa Serikali kuruhusu mitihani hiyo isahihishwe upya ili ukweli halisi upatikane.

Kwa mujibu wa Kiyeyeu, kama matokeo hayo yataachwa kama yalivyo, wanafunzi wengi wataharibikiwa maisha, wakiwamo wanaotoka katika familia masikini.

”Tunakuomba Mwenyekiti uzungumze na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi (Dk. Shukuru Kawambwa) ili mitihani yetu isahihishwe upya na wale wanaotaka kurudia mitihani yao wagharamiwe na Serikali, kwa vile vituo vinavyotoa huduma hiyo vinatoza gharama kubwa kuliko uwezo wetu,” alisema Upendo.

Naye Upendo Vitus aliyehitimu katika Shule ya Sekondari Tagamenda, alimwambia Mwenyekiti huyo wa CCM, kwamba wanachotaka wao Serikali iruhusu mitihani isahihishwe upya ili ukweli ujulikane.

Alisema kwamba haoni umuhimu wa tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa kuwa haitakuja na majibu yanayoaminika.

Kutokana na hali hiyo, alisema kinachotakiwa ni Serikali kukubali mitihani hiyo isahihishwe upya, ikiwa ni pamoja na kugharamia masomo kwa watakaotaka kurudia kidato cha nne mwaka huu.

Naye Msambatavangu alipokuwa akizungumza katika mkutano huo, aliwataka wanafunzi hao kutoyumbishwa na kauli za wanasiasa, kwa kuwa wanasiasa wanaweza kuwatumia vibaya kupitia matokeo mabaya ya kidato cha nne.

Pia, aliwataka baadhi yao waliokuwa na mawazo ya kujiua, wasifanye hivyo japokuwa wazazi wao wanawasema vibaya baada ya kufeli mtihani huo.

”Hakika hamtajuta kwa uamuzi huu niliouchukua wa kukutana na nyie kwa sababu nimeumia sana moyoni mwangu na nikalazimika kusema lazima kuna kitu kifanyike kwa ajili yenu.

”Nimeshafanya mazungumzo na baadhi ya vyuo vikuu vya hapa kama Tumaini na RUCO ili waangalie namna ya kuwasaidia kwa kuandaa kozi za muda mfupi hadi mwezi Mei mwaka huu.

”Lengo la kuandaa kozi hizi ni kuwanoa ili baadaye tuone kama wapo wanaoweza kusaidiwa kwa kuendelea na elimu ya ngazi ya cheti.

”Najua kuna wanasiasa pamoja na wanaharakati watajiingiza katika hili, lakini tambueni kwamba, huu siyo wakati wa wanasiasa, wanaharakati na wadau wa elimu nchini kupigana mawe kutokana na anguko hili.

”Ila kinachotakiwa hapa ni Serikali ya CCM na watendaji wake, kujipanga upya na kutazama ni kwa namna gani kundi la wanafunzi waliofanya vibaya katika mitihani yao wanaweza kusaidiwa.

”Nayasema haya kwa sababu inawezekana mliopata sifuri na kuonekana hamna maana, mkawa kioo katika maisha na waliowacheka na kuwabeza, wakawaheshimu kutokana na mchango wenu katika elimu hapo baadaye.

”Nawaomba sana msikate tamaa, maisha ni safari ndefu kwa sababu kufeli mitihani si kufeli maisha, unaweza ukafeli mtihani lakini kwa kuwa Mungu ana mipango yake kwa kila mtu, unaweza kuwa mtu wa maana kuliko hata yule aliyefaulu,” alisema Msambatavangu.

Naye Mkurugenzi wa Kozi Fupi na Masomo Endelevu katika Chuo cha RUCO, Baby Chuma, aliwataka wanafunzi hao kutokata tamaa kwa kuwa kufeli kidato cha nne siyo kufeli maisha.

Aliwataka pia wajiendeleze kwa kujiunga na kozi mbalimbali za masomo ili baada ya miaka miwili, wawe na sifa ya kujiunga na vyuo vikuu.

Katika utekelezaji wa suala hilo, alisema menejimenti ya RUCO, imeshakubaliana na kiongozi huyo wa CCM ili kozi fupi zitolewe kwa waliofeli mitihani hadi Mei mwaka huu.

Kwa upande wake, Msajili wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini (IUCo), Melckzedeck Nduye, aliwahakikishia wanafunzi hao, kwamba chuo hicho kimeungana na wadau wengine kutoa huduma kwa wanafunzi waliofeli kuanzia Machi, mwaka huu.

Wakati hao wakisema hayo, Mratibu wa Uhamasishaji wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), Wilaya ya Iringa, Aidan Salehe, alipoulizwa kuhusu matokeo hayo ya kidato cha nne, alisema baraza hilo limepanga kuwaunganisha wanafunzi hao kwa kuitisha maandamano ya kulaani matokeo hayo.

”Maandamano yako pale pale, mazingira mabovu ya elimu, mitaala mibovu na uongozi wa aina hii, ndio tunataka vijana wausemee wenyewe.

”Katika hili alichokifanya Mwenyekiti wa CCM ni kizuri kabisa na kinapaswa kupongezwa, lakini ukweli ni kwamba, ameamua kuwakutanisha waliofeli kwa sababu anajua tukiandamana tunaweza kuchota wanachama wengi zaidi wakiwamo wa CCM,” alisema Aidan.

Katika matokeo hayo ya kidato cha nne yaliyotangazwa wiki iliyopita, Mikoa ya Iringa na Njombe ilikuwa na wahitimu 15,428, lakini asilimia 89 walipata alama sifuri.

Wakati akitangaza matokeo hayo, Dk. Kawambwa alisema watahiniwa 480,036 walisajiliwa nchini kote kufanya mtihani lakini waliofanya mtihani ni 397,136. Pia alisema jumla ya watahiniwa 126, 847 kati ya 397,136 waliofanya mtihani huo wamefaulu huku watahiniwa 270,289 hawakufaulu.

Katika matokeo hayo, alisema waliopata daraja la kwanza ni 1,641, daraja la pili ni 6,453, daraja la tatu ni 15,426, na darala la nne ni 103,327.
.
Kampuni ya Nokia imezindua simu yake mpya ya mkononi ambayo ukiichaji mara moja tu, unaendelea kuitumia bila kuichaji kwa siku 35.. ni simu ambayo inatarajiwa kupata soko kubwa sana kwenye sehemu ambazo kuna tatizo la umeme na pia inaweza kutumika kama back-up phone.
Simu hii ya Nokia 105 inatarajiwa kuingia sokoni ndani ya wiki chache zijazo ikiwa na mvuto kama colour screen, ina tochi na inashika Fm Radio na gharama yake ni ndogo sana pia.
.

Utafiti: Dk Slaa aongoza vinara tisa urais 2015

Utafiti: Dk Slaa aongoza vinara tisa urais 2015




WAKATI baadhi ya wanasiasa wakiwa wameanza kujiwinda kwa ajili ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Shirika la Utafiti la Synovate limetoa matokeo ya utafiti wake ambao unaonyesha vigogo tisa kuwamo katika mchuano huo.
Utafiti huo umeonyesha kuwa endapo uchaguzi huo ungefanyika sasa, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi baada ya kuongoza orodha hiyo akipata asilimia 17.


Katika matokeo ya utafiti huo uliofanywa Desemba mwaka jana, Dk Slaa anafuatiwa kwa mbali na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amefungana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kila mmoja akipata asilimia tisa.

Hata hivyo, licha ya kuongoza, Dk Slaa ameporomoka kwa asilimia 25 ikilinganishwa na matokeo ya utafiti kama huo uliofanywa na taasisi hiyo mwaka 2011 ambapo alipata asilimia 42.

Kadhalika, umaarufu wa Pinda ambaye anaongoza miongoni mwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeshuka kwa asilimia tatu kutoka 12 za mwaka juzi, wakati Zitto ameendelea na kiwango kilekile cha asilimia tisa alizopata katika utafiti uliotangulia.
Wengine wanaofuata na asilimia walizopata kwenye mabano ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli (8), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (7) na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (5).

Pia wamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (4) ambaye amefungana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (4) na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (2).
Ikilinganishwa na utafiti wa 2011, Lipumba ameporomoka kwa asilimia tisa.
Lowassa amepanda kwa asilimia sita, Dk Magufuli asilimia nne, Mbowe na Membe wamepanda kwa asilimia mbili kila mmoja, wakati Sitta amebaki katika kiwango kilekile cha asilimia mbili.

Hata hivyo, utafiti huo umeonyesha kuwa wananchi ambao hawana uamuzi wa kuchagua mtu yeyote kati ya hao kwa sasa ni asilimia 18, likiwa ni ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa na utafiti uliotangulia.
CCM yatamba
Katika utafiti huo, CCM kimeonyesha kuwa ni chama ambacho asilimia 52 ya wananchi wangependa kujiunga nacho, kikiwa kimepanda chati kwa asilimia moja kutoka asilimia 51 mwaka jana.

Kwa upande wa Chadema, wananchi ambao wanapenda kujiunga nacho imeshuka kutoka asilimia 35 mwaka 2011 hadi 31 mwaka jana.

Uwezekano mkubwa wa CCM kupanda chati ni kutokana na ukweli kuwa mwaka jana kilikuwa na uchaguzi ulioanzia ngazi ya mashina hadi taifa na kuibua vuguvugu kubwa masikioni mwa wananchi.

Chadema hakikuwa na harakati kubwa za kisiasa ukiacha kampeni ya Movement For Change (M4C), ambayo kwa kiasi haikuwa na pilika kama uchaguzi wa CCM.
Chama kingine ni CUF ambacho kimeporomoka kwa kupata asilimia 10 mwaka 2011 hadi nne mwaka 2012.

Hata hivyo, asilimia ya wananchi kutokutaka kujihusisha na chama chochote imepanda kutoka asilimia mbili mwaka 2011 hadi 12 mwaka 2012.
Rushwa
Katika suala la rushwa nchini, utafiti huo umeonyesha kuwa kati ya watu 10 waliohojiwa, wanne walikuwa na maoni kuwa rushwa imeongezeka kufikia asilimia 41, asilimia 30 walisema iko palepale, asilimia 23 walisema imepungua na asilimia tano hawajui.

Monday, February 25, 2013

MITAALA NI CHANZO CHA WANAFUNZI KUFELI

MITAALA


Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa,  akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam juzi, baadhi ya vitabu vya mitaala batili iliyochangia kufelisha wanafunzi wa Kidato cha Nne, Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi wa chama hicho, Bw. Faustine Sungura.

PINDA AUNDA TUME YA KUCHUNGUZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Bushiri, iliyopo Wilaya ya Pangani mkoani Tanga, Mpaji Said (20), akiwa amelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo, akipatiwa matibabu baada ya kudaiwa kunywa sumu ya panya, kutokana na fedheha aliyoipata kwa kutofaulu mtihani wa taifa wa kidato cha nne. Picha na John Senmkande 

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameunda tume itakayochunguza sababu za idadi kubwa ya wanafunzi wa kidato cha nne kuvurunda katika matokeo ya mtihani huo yaliyotangazwa hivi karibuni.
Katika matokeo hayo ambayo yanatajwa kuwa mabovu kuliko yoyote yaliyowahi kutokea katika historia ya Tanzania, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani huo walipata daraja sifuri.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo alisema kuwa tume hiyo inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki ijayo, ambapo itajumuisha Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi.
Lyimo aliwataja wadau wengine watakaohusika katika uchunguzi huo kuwa ni kutoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (Tahossa)
“Tume hiyo itahusisha asasi zisizo za kiserikali (NGOs), zinazojishughulisha na masuala ya elimu. Wazazi, walezi na wananchi wote kwa jumla watoe ushirikiano kwa tume, ili ifanye kazi kwa ufanisi,” alisema Lyimo.
Akizungumzia hatua hiyo ya Pinda, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema) alisema wazo hilo ni zuri, lakini kuunda tume bila utendaji hakutakuwa na maana katika elimu nchini.
Alisema kuwa tume nyingi zimeundwa, lakini hakuna tume iliyowahi kuleta mabadiliko na kwamba mara nyingi matokeo ya uchunguzi huwa ni ya kuidhalilisha Serikali.
Msigwa aliongeza kuwa tume hizo hutumia fedha za wananchi na matokeo yake hayatangazwi wala kufanyiwa kazi.
“Serikali ingewaita wadau wa elimu na kuzungumza nao ijue wapi penye matatizo. Halafu maelezo ya wadau hao yajadiliwe bungeni,” alisema Msigwa akiitaka Serikali kuacha kuchanganya ushabiki wa kisiasa pindi zinapowasilishwa hoja muhimu za maendeleo ya taifa na kuongeza:
“Juzi hoja ya Mbatia imetupwa kapuni, hata sisi wabunge tunapeleka hoja nyingi, lakini hazifanyiwi kazi, kwa sababu ya ushabiki.”
Kiongozi wa Jukwaa la Katiba nchini, Profesa Issa Shivji aliwataka Watanzania wasubiri kuona tume hiyo itafanya nini.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Benson Bana, alitaka suala la elimu lisichukuliwe kisiasa, badala yake Serikali itatue kero za elimu, alizosema zinajulikana na kwamba hakuna haja ya kumtafuta mchawi.
“Kwa nini tupoteze fedha za walipa kodi kwa kuunda tume, tume itachunguza nini wakati wanafunzi wameshafeli?” alisema akihoji Profesa Bana.
Aliongeza: “Sioni haja ya tume, kinachotakiwa kufanywa ni kuchukua hatua kali tu.”