Kondomu feki zaanza kuleta madhara Uingereza
Kwa ufupi
Zaidi ya kesi 21, 000 za maambukizi mapya zimedaiwa kutambulika kwa mwaka 2011/12.
WAKATI kondomu feki zilizopigwa marufuku
Uingereza mwaka jana zikiwa katika mzunguko nchini Tanzania, kesi za
gonjwa la ngono hatari lisilotibika zimeongezeka kwa asilimia 25
Uingereza, huku wataalamu wakionya kwamba ugonjwa huo umekuwa sugu zaidi
katika tiba.
Zaidi ya kesi 21, 000 za maambukizi mapya zimedaiwa kutambulika kwa mwaka 2011/12.
Kondomu hizo feki aina ya Trojan na Durex zenye
vipele vipele ambazo mwishoni mwa mwaka jana serikali ya Uingereza
iliingia katika msako mkali kusaka mamilioni ya kondomu hizo bandia
zilizokuwa zikiuzwa nchini humo miezi 18 iliyopita.
Kirusi kinachoambukiza ugonjwa huo hatari
kimetajwa kuwa ni 'Neisseria' ambacho ni tofauti na vingine ambavyo mara
nyingi hutibiwa kwa dozi moja tu ya viuavijasumu (antibiotics) ambayo
angalau hufanya kazi kwa asilimia 95 kiufanisi.
Akizungumzia maendeleo ya utafiti wa kondomu hizo
nchini , Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Wiwango Tanzania(TBS),Leandri
Kinabo alisema shirika hilo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Ckula na
Dawa(TFDA) hivi sasa lipo katika mchakato wa kuhakikisha vipimo halisi
vya ubora wa bidhaa hizo vinaangaliwa.
"Hili suala ni nyeti na ni la kiafya na usalama
zaidi, hivyo tulikaa kikao na TFDA na tulikubaliana tufanye uchunguzi wa
kondom hizi, kwani ni kweli zipo sokoni lakini suala la ubora
linatakiwa kuangaliwa," alisema Kinabo.
Aliwataka Watanzania kuwa na subira ili waweze
kuchunguza bidhaa hizo kwa umakini zaidi na kwamba baada ya uchunguzi
watatoa majibu.
Baada ya gazeti hili kutaka kujua uhalali wa
bidhaa hizo sokoni, Kinabo alisema bidhaa zote zinazoingia bandarini
hupimwa, lakini kuna baadhi ya bidhaa ambazo huingizwa kwa njia zisizo
halali na mara nyingi huwa feki.
"Inetegemea na lebo ya bidhaa husika, kuna wakati
bidhaa inaweza kupimwa na kuonekana kuwa ni salama na kisha kuingizwa
sokoni, lakini baada ya muda zikaingia bidhaa feki zenye nembo hiyohiyo,
hivyo hilo ni suala la kusubiri vipimo kutoka TFDA," alisema Kinabo.
Tatizo hilo sugu Uingereza limesababishwa
kuanzishwa kwa kampeni mpya ya kukabiliana na tishio kubwa la kuongezeka
kwa kasi kwa magonjwa hayo nchini Uingereza na Wales ambayo yamedaiwa
kusambaa kwa wingi nchini humo na nchi zinazoendelea.
Wataalamu wa Afya wana matumaini mapya baada ya
kuanzishwa mpango mkakati wa kuzuia ugonjwa wa gono 'Gonorrhoea
Resistance Action Plan' ambayo itaongeza ufahamu wa ugonjwa huo.
Mpango huo ulioanzishwa na shirika la Ulinzi wa
Afya, utafuatilia tatizo hilo la kimataifa linaloongezeka kwa kasi tangu
kupungua miaka 10 iliyopita.
No comments:
Post a Comment